Faraja Kotta (amezaliwa
6 Mei 1985,
Dar es Salaam) alikuwa mrembo wa
Tanzania mwaka
2004.
Kotta ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto wanne.
Elimu yake ya msingi aliipata katika shule ya msingi Olympio iliyopo jijini
Dar es Salaam, baadae kujiunga na shule ya sekondari St Francis iliyoko mkoani Mbeya kisha kuendelea na
elimu ya kidato cha 5 na 6 katika shule ya sekondari ya St Marys Mazinde Juu , iliyoko
Lushoto,
Tanga, Tanzania.
Historia ya Urembo
Kotta aliwahi kuwa "Miss
Ubungo" na baadae kuwa "Miss
Kinondoni", baada ya kuwa Miss
Kinondoni akaja kuchaguliwa kuwa "Miss
Tanzania" kwa mwaka wa
2004.
Kazi Tofauti na Urembo
Kotta ni Mwachama wa "Youth Executive Committee" ambayo ipo chini ya
Youth Net Tanzania,
na pia ni Program Officer wa kipindi cha Njia Panda ambapo anafuatilia
wale wananchi wanaojitokeza na matatizo na kuhakikisha wamesaidiwa na
vipi wanaendelea.
Maisha Binafsi
Faraja hivi karibuni tarehe 30 novemba 2007 amefunga ndoa na mbunge wa
Singida mheshimiwa
Lazaro Nyalandu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni